Makonda amkabidhi majukumu ya Ofisi RC mpya

Leo Juni 30,2025, aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amekabidhi ofisi kwa mkuu mpya wa mkoa huo Kenan Kihongosi. 

8Hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan alifanya mabadiliko kwenye nafasi mbalimbali za uongozi, ambapo alimuhamisha Kenan Kihongosi kutoka kuwa mkuu wa Mkoa wa Simiyu kuwa mkuu wa Mkoa wa Arusha kuchukua nafasi ya Makonda. 

Makonda amejitosa kwenye kinyan'ganyiro cha Ubunge, ambapo tayari amechukua fomu kuwania Ubunge katika Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii