Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla, amesema idadi ya Wanachama wa CCM waliojitokeza kuchukua imekuwa kuliko wakati wowote ambapo kwa ubunge na udiwani takribani Watu elfu 20 wamechukua fomu ikiwemo Watu 4109 waliochukua fomu za Ubunge majimboni.
Akiongea Jijini Dar es salaam leo July 03,2025, Makalla amesema “Watu wengi wamechukua fomu kwa takwimu tu za haraka haraka waliochukua fomu katika Majimbo yote Tanzania Bara waliochukua fomu katika Majimbo ni Watu 3585 na kule Zanzibar katika Majimbo wamechukua 524 kwahiyo katika Majimbo tuna Wanachama walioonesha nia wapo 4109 na tuna Majimbo 272 kwahiyo utaweza kuona namna gani hamasa ilivyo kubwa”
Kwa upande wa Uwakilishi kule Zanzibar wamechukua fomu Wanachama 503, UWT wao wamechukua 623 Bara na ndani yake wapo 91 wa Makundi maalum lakini kule Zanzibar wamechukua 8 na viti maalum uwakilishi 9 kwahiyo jumla UWT waliojitokeza ni 640
Umoja wa Vijana wamechukua 161 kwa maana katika UVCCM wapo 154 na Zanzibar wapo 7 kwahiyo unakuta jumla 161, Jumuiya ya Wazazi Bara wamechukua 55 na Zanzibar Ubunge viti maalum watatu na uwakilishi wanne kwahiyo jumla
Wazazi wapo 62 ubunge na uwakilishi, kwahiyo kwa jumla ubunge na uwakilishi waliochukua fomu ni 5475”
“Nafasi za udiwani bado wanaendelea kuchakata lakini wameniambia katika Kata 3960 tunaweza kuwa na Wagombea zaidi ya elfu 15, kwahiyo CCM tuna Wanachama waliojitokeza katika nafasi za ubunge na udiwani kufikia elfu 20, ni idadi kubwa ya idadi ya waliojitokeza kuliko wakati wowote”