Watuhumiwa mauaji ya kijana kwa kipigo wanaswa Geita

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limewakamata watu wawili akiwemo Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Liyobahika, Ferdinand Antony kwa tuhuma za mauaji ya kijana Enock Mhangwa, huku  watuhumiwa wengine watatu wakiwemo mgambo wakiendelea kuwatafuta.

Taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi waliyoitoa leo Julai 4, 2025  ni kutokana na picha mjongeo inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii  ikiwaonyesha watuhumiwa hao wakiwa wamemfunga mikono Enock na kumpeleka porini na kuanza kumpifa kwa kutumia fimbo sehemu mbalimbali mwilini.

Jeshi la Polisi limetoa ufafanuzi wa picha mjongeo ambayo inaonekana kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha kijana aliyefungwa mikono huku akipigwa kwa fimbo.

"Tukio hilo lilitokea Juni 26, 2025 hivyo, kutokana na kushambuliwa kwa kipigo, kijana huyo anayejulikana kwa jina la Enock Mhangwa alifariki dunia," imeeleza taarifa hiyo ya Polisi.

Jeshi la Polisi limesema tayari limewakamata  watuhumiwa wawili wanaodaiwa kuhusika katika mauaji hayo, ambao mmoja ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Liyobahika na Hussein Madebe.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii