Mkataba wa kihistoria kati ya DRC na Rwanda mwisho miaka 30 ya Vita

 Rais wa Marekani Donald Trump amebainisha Julai 9 mwaka huu ili kutiwa saini kwa makubaliano ya amani kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Rwanda mwishoni mwa mwezi wa Julai. Kulingana rais wa Marekani, hati hii itatiliwa saini mjini Washington na Marais Félix Tshis  ekedi na Paul Kagame.

Ameeleza kuwa imani yake ni kwamba wiki mbili zijazo, viongozi wa nchi zote mbili watakuja kutia saini makubaliano ya mwisho. Wiki iliyopita, tuliwapokea mawaziri wa mambo ya nje, na sasa tutaadhimisha mwisho wa vita vya kutisha vilivyodumu kwa miaka 30. Nimesoma makala, nimesikia shuhuda, na ulikuwa mzozo wa kutisha." Getty Images via AFP - ANDREW HARNIK.

Makubaliano hayo yanalenga kumaliza miongo mitatu ya vita vilivyosababisha vifo vya watu wengi mashariki mwa DRC, ambapo Rwanda inashutumiwa kuwaunga mkono waasi wa M23 kupitia kutumwa kwa wanajeshi wake mashariki mwa DRC.

Katika hafla hii, Donald Trump alisifu jukumu muhimu lililofanywa na mshauri wake mkuu kwa Afrika, Massad Boulos, ambaye alimshukuru kwa mchango wake katika mafanikio haya ya kidiplomasia, ambayo kwa muda mrefu yalionekana kuwa hayawezekani.

Pia alitangaza: "Ninaamini kwamba katika wiki mbili zijazo, viongozi wa nchi zote mbili watakuja kutia saini makubaliano ya mwisho. Wiki iliyopita, tuliwapokea mawaziri wa mambo ya nje, na sasa tutaadhimisha mwisho wa vita vya kutisha vilivyodumu kwa miaka 30. Nimesoma makala, nimesikia shuhuda, na ulikuwa mzozo wa kutisha."

Mnamo tarehe 27 Juni, mawaziri wa mambo ya nje wa DRC na Rwanda walikwenda Ikulu ya White House kwa ajili ya kutia saini hati hii. Walisisitiza kwamba mzozo huu uliodumu kwa miongo mitatu, ulisababisha vifo vya karibu watu milioni 7—idadi ambayo inaweza kuwa kubwa zaidi.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii