ACT kutoridhishwa na uongozi wa Mbunge jimbo la Same Mashariki

Chama cha ACT Wazalendo kimeonesha kutoridhishwa na namna Mbunge wa Same Mashariki mkoani Kilimanjaro, Bi. Anne Kilango Malecela anavyolihudumia jimbo lake kikisema kuwa alitoa taarifa za uongo bungeni kuhusu uwepo wa viwanda vya tangawizi jimboni humo, kinyume na uhalisia uliopo kwa wananchi.

Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika jimbo hilo, Naibu Mwenezi wa Taifa wa ACT Wazalendo, Shangwe Ayo, amesema hakuna viwanda vya namna hiyo vilivyojengwa, licha ya kauli ya Mbunge huyo aliyodai kuwa tayari amevijenga.

Shangwe ameendelea kushutumu utendaji wa Mbunge huyo kwa kile alichodai kuwa ni kutumia mabango ya kisiasa badala ya kufanya kazi za maendeleo.

“Same imejaa mabango ya ‘Mama ana upiga mwingi’. Lakini hali ya maendeleo ni duni. Mabango ni mengi kuliko huduma”, amesema.

Viongozi wa ACT pia walitumia jukwaa hilo kuwataka wananchi wa Same Mashariki kuukataa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakisema chama hicho kimekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya wananchi wa eneo hilo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii