Kesi ya kusababisha madhara mwilini inayowakabili wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Mary Matogolo (22) na wenzake wawili itatajwa leo Julai 14 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mary na wanafunzi wenzake wanakabiliwa na mashitaka tisa, likiwemo la kutishia kuua, kutoa taarifa za uongo mitandaoni na uharibifu wa mali za mwanafunzi mwenzao.
Mbali na Mary, wanafunzi wengine katika kesi hiyo ni Ryner Mkwawili wa Chuo Kikuu Ardhi Dar es Salaam (ARU) na Asha Juma, wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Dar es Salaam (TIA).
Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu Aaron Lyamula na leo Julai 14, 2025 imepangwa kwa ajili ya kutajwa na kuangalia iwapo upelelezi wa shauri hilo umekamilika au laa.
Hata hivyo washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.