Chaumma yapata watia nia majimbo yote mkoani Mara

Mratibu wa Uchaguzi na Kampeni wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Kanda ya Serengeti Catherine Ruge ametangaza kupatikana kwa watia nia wa ubunge katika majimbo yote 10 ya mkoa wa Mara akieleza kuwa hamasa imekuwa kubwa kwa wananchi wa mkoa huo kujitokeza kuchukua fomu za kugombea udiwani na ubunge kupitia chama hicho.

Akizungumza siku ya Jumatatu wakati wa hafla ya kutoa taarifa fupi ya watia nia wa mkoa wa Mara, Ruge ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na Uchumi wa CHAUMMA taifa, ameeleza kuwa katika kata 179 za mkoa wa Mara, chama hicho kimepata watia nia katika kata 90.

"Ninaposema CHAUMMA tuko 'serious', hiko ndicho ninachomaanisha. Kwenye mkoa wa Mara tayari tuna watia nia kwenye majimbo yote. Kati ya kata 179, tuna watia nia wa udiwani 90, hii siyo kazi ndogo. Kwahiyo tutaendelea kufanya kazi, kuhamasisha na kushawishi watu wajitokeze, waweze kuchukua fomu za kutia nia kugombea nafasi za udiwani na ubunge.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii