Maambukizo ya kipindupindu yaendelea kuripotiwa jijini Kinshasa

Maambukizo ya kipindupindu bado hayadhibitiwa katika jiji kuu Kinshasa nchini DRC huku mamlaka katika jimbo jirani la Maï-Ndombe, ikithibitisha ugonjwa huo ambao kwa miezi kadhaa sasa umeendelea kusambaa kwa kasi katika maeneo mbalimbali.

Watu wamezuiliwa kuingia katika eneo ambapo wagonjwa wanazuiliwa kupokea matibabu. Karibia wagonjwa 25 wakiwasili kupokea matibabu. Wengi wa wagonjwa ni watoto.  Dkt Francis Kabole anawahudumia.

“Tuna watenga iliwasiwaambukize wengine. Tangu tarehe saba tulianza kupokea wagonjwa. Kwa siku tumepokea kesi kumi au kumi na tano. Walio hapa ni watoto wa chini ya miaka kumi.” alisema Dkt Francis Kabole.

Gavana wa jimbo hilo Nkoso Kevanie, amesema, miongoni mwa sababu za vifo ni kuchelewa kuwasili kwa wagonjwa hospitalini na ukosefu wa maji safi ya kunywa, huku akiwataka raia kuzingatia hatua za kujikinga. 

“Tuna zaidi ya kesi zaidi ya 238 ambazo zimethibitishwa na vifo zaidi ya 30 vimerekodiwa. Maeneo ya Bolobo, Mushi, Nyuki, na Kwamouth yameathirika zaidi. Nimeomba watu wote kuzingatia hatua muhimu kama vile kuosha mikono na sabuni au jivu, kutumia chakula ambacho kimeiva vizuri, kutumia maji safi, wasinawe au kufua ndani ya ziwa Maï-Ndombe.”

Kampeni za uhamasishaji zimetolewa kwa wakaazi wa eneo hilo. Hélène Kyesse anaelezea hatua anazochukua baada ya kijana wake kuambukizwa Kipindupindu.

DRC imeripoti visa Elfu 33 na Mia tano vya maambukizo ya kipindupindu katika majimbo 17, miongoni mwa 26.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii