Donald Trump aipa Urusi siku 50 kumaliza Vita nchini Ukraine

Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye kwa mara nyingine ameonyesha kusikitishwa kwake kutokana na tabia ya mwenzake wa Urusi Vladimir Putin mnamo Jumatatu, Julai 14, ameipa Urusi siku 50 kumaliza vita la sivyo itakabiliwa na vikwazo vikali, na akatangaza kukaribia kusafirisha idadi kubwa ya silaha kwenda Ukraine kupitia NATO. Kwa kufanya hivyo, rais wa Marekani ameonyesha wazi kuwa subira yake kwa rais wa Urusi imefikia mwisho.

Rais Donald Trump ametangaza Jumatatu, Julai 14, kwamba angeiadhibu Urusi kwa ushuru wa forodha ikiwa hakutakuwa na makubaliano ya kumaliza vita vya Ukraine ndani ya siku 50, mfano wa hivi punde zaidi wa kuchanganyikiwa kwake kutokana na Rais wa Urusi Vladimir Putin. Trump ametoa tangazo hili wakati wa mkutano katika Ofisi ya Oval na Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte.

"Tutaweka ushuru mkubwa sana ikiwa hatutafikia makubaliano ndani ya siku 50," rais wa Marekani ametangaza. Amebainisha kuwa huu utakuwa "ushuru wa pili," akimaanisha kuwa ungelenga washirika wa biashara wa Urusi ili kuitenga Moscow katika uchumi wa dunia. "Ninatumia biashara kwa mambo mengi," Trump ameongeza. "Lakini ni bora kwa kutatua migogoro." "Kama hatutakuwa na makubaliano ndani ya siku 50, ni rahisi sana, (ushuru) utakuwa 100%, na ndivyo hivyo," ameongeza.

Nchi za Ulaya kununua kww "mabilioni na mabilioni" ya dola silaha za Marekani

Mbali na tishio la ushuru, Donald Trump na Mark Rutte walijadili mradi wa kisasa wa mtandao wa silaha wa Marekani. Washirika wa Ulaya wanapanga kununua vifaa vya kijeshi na kisha kuvituma Ukraine. Donald Trump amesema ununuzi huu utafikia "mabilioni na mabilioni" ya dola. Trump amesema amefurahishwa kuona Ulaya ikitumia gharama kubwa zaidi katika ulinzi baada ya wanachama wengi wa NATO, katika mkutano wa hivi majuzi huko Hague, kukubaliana kuongeza matumizi hadi 5% ya Pato lao la Taifa. "Wajimbi wao ni wa ajabu," Trump amesema. "Mwisho wa siku, kuwa na Ulaya yenye nguvu sana ni jambo zuri," ameongeza.

Mark Rutte amesema UjerumaniFinlandCanadaNorwaySwedenUingereza, na Denmark zitakuwa miongoni mwa wanunuzi wanaowezekana wa silaha zitakazotumwa Ukraine. Ameongeza kuwa "kasi ni jambo la msingi hapa" na kwamba uwasilishaji huu unapaswa kumtia moyo Putin "kufikiria upya" mazungumzo ya amani.

"Hili ni jambo kubwa sana ambalo tumefanya. Vifaa vya kijeshi vya thamani ya mabilioni ya dola vitanunuliwa kutoka Marekani, kwenda NATO, nk., na vitasambazwa kwa haraka kwenye uwanja wa vita," rais wa Marekani amesema. Amebainisha hasa kwamba mifumo ya ulinzi wa anga ya Patriot itatolewa kwa Ukraine "katika siku zijazo."

"Hii ina maana kwamba Ukraine itakuwa na kiasi kikubwa sana cha vifaa vya kijeshi, kwa ulinzi wa anga, lakini pia makombora na silaha," aliongeza Katibu Mkuu wa NATO.

Zelensky anasema alizungumza na Trump na kujadili "suluhisho" za kuilinda Ukraine

Siku ya Jumatatu ,  wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kwamba alizungumza na Donald Trump na kwamba walijadili "suluhisho" za kuilinda vyema Ukraine, baada ya mwenzake wa Marekani kuidhinisha kupelekwa zaidi kwa silaha huko Kyiv.

"Tulijadiliana na Rais (Trump) njia na suluhu zinazohitajika kulinda zaidi raia dhidi ya mashambulizi ya Urusi na kuimarisha misimamo yetu," Volodymyr Zelensky amesema katika ujumbe kwenye X.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii