Jeshi la Polisi linamshikilia Samwel Kayoka (16) Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza Shule ya Sekondari Mtenga kwa tuhuma za mauaji ya mdogo wake Jackson Kayoka (14) baada ya kumpiga fimbo kichwani walipokuwa wakicheza mchezo wa kupigana kwa fimbo.
Kamanda wa Polisi Mkoa SACP Shadrack Masija amesema tukio lilitokea Julai 7 mwaka huu Kijiji cha Mtenga ‘A’ Wilayani Nkasi ambapo kwa sasa uchunguzi unaendelea na Samwel atafikishwa Mahakamani baada ya taratibu kukamilika.
Afisa Mtendaji wa Kijiji Romwald Kapele amesema Watoto hao ni wa familia moja na kuwa walichokuwa wanafanya ni jambo la kawaida katika mazingira ya mila zao Watoto kucheza kwa kupigana kwa fimbo