Serikali yaimarisha vituo vya ununuzi madini kutoka 61 hadi kufikia 109

Serikali imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha usimamizi na uendelezaji wa sekta ya madini na  kuimarisha masoko na minada ya uuzaji madini, ambapo vituo vya ununuzi wa madini vimeongezeka kutoka vituo 61 Novemba, 2020 hadi 109 mwaka huu, na masoko ya madini yameongezeka kutoka

41 hadi 43.

Wakati Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani mauzo ya madini nje yalifikia thamani ya $3,116.40milioni sawa na kiasi cha kilogramu 48,400 miaka minne ya Rais Dkt. Samia, mauzo yamefikia jumla ya $4,119.9milioni sawa na TZS10.712Trilioni sawa na kiasi cha kilogramu 60,000 mwaka 2024.

Serikali ya Dkt Samia imeisimamia sekta hii na kuiwezesha kuongeza mchango wake katika Pato la Taifa kutoka asilimia 6.8 mwaka 2020, hadi kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2025.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii