Wadau wa elimu nchini wamependekeza kuchukuliwa hatua madhubuti kuhusu suala la wizi wa mitihani, ambalo limeonekana kuanza kuota mizizi na kuathiri kwa kiasi fulani uhalali wa matokeo ya mitihani ya taifa.
Wakieleza kuwa vitendo hivyo vimechangia baadhi ya watahiniwa kufutiwa matokeo yao, hali inayoathiri mustakabali wa wanafunzi wengi.
Mapendekezo hayo yanakuja wakati ambapo Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita kwa mwaka huu, ambapo jumla ya watahiniwa waliofaulu ni 125,779, sawa na asilimia 99.95 huku watahiniwa 68 pekee, sawa na asilimia 0.05, walishindwa kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali.