kushambuliwa kwa Padri Charles Kitima linafahamika vizuri na vyombo vya dola

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dkt. Charles Kitima, amesema tukio la yeye kushambuliwa na watu wasiojulikana linafahamika vizuri na vyombo vya dola, na kwamba hatua zaidi kuhusu uchunguzi na haki zipo katika vyombo hivyo vya usalama.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na vyombo vya habari Padri Kitima amesema kuwa tayari amehojiwa na maofisa wa usalama ambao walipata maelezo yake, na sasa anasubiri hatua zao.

Ameeleza kuwa haitakuwa vyema kwa vyombo vya dola kufanya kwa Watanzania wengine kile alichokumbana nacho yeye, na ameonesha masikitiko yake kuhusu ukimya wa kisheria licha ya tukio hilo kujulikana vyema kwa mamlaka husika.

Asingependa mtanzania yeyote vyombo vinavyolifanya kazi suala langu wanavyomfanyia yeye wafanyie wengine hivyo asingependa wafanye hivyo kwasababu kama watu wanalijua tukio, na huoni kinachoendelea asingependa wengine wakosewe kiasi hicho.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi Padri Kitima alishambuliwa na watu wawili wasiojulikana usiku wa Aprili 30 mwaka huu akiwa njiani kuelekea maliwatoni katika makazi yake yaliyopo Kurasini, Dar es Salaam. Alijeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Aga Khan, ambako alitibiwa na kuruhusiwa baadaye.

Mnamo Mei 25, 2025 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kupitia taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro, lilieleza kumshikilia Rauli Mahabi/ Haraja, mkazi wa Kurasini, kwa tuhuma za kuhusika katika shambulio dhidi ya Kitima na kwamba lililenga kumfanyia mahojiano.

Zaidi taarifa ya mwisho ya jeshi hilo iliyotolewa Mei 31, 2025 ilieleza kuwa lingemfanyia mahojiano Padri Kitima ili lipate maelezo ya kimaandishi ili yaende Ofisi ya Mwendesha Mashtaka kabla ya kutoa taarifa rasmi juu ya tukio hilo.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii