Kabila aripotiwa kupinga mkataba wa uchimbaji madini kati ya DRC na Marekani

Rais wa zamani wa DRC, Joseph Kabila ameripotiwa kupinga mkataba wa uchimbaji madini kati ya DRC na Marekani baada ya Washington, kufanikisha makubaliano kati ya Kinshasa na Kigali.

Rais Kabila anaripotiwa kuwa na mtazamo tofauti kuhusiana na mkataba wa Marekani, wakati huu akiripotiwa kukamilisha mazungumzo yake na viongozi wa tabaka mbalimbali mashariki mwa DRC, hasa katika miji ya Goma na Bukavu, kuhusu mustakabili wa taifa.

Kwa mujibu wa wandani wa Kabila ambao RFI ilifanikiwa kuzungumza nao, rais Kabila ameandaa ripoti ambayo atawasilisha kwa mazungumzo ya kitaifa yanayotarajiwa na mbayo yatasimamiwa na kanisa Katoliki na lile la Protestanti.

Watu wa Karibu wa kiongozi huyo wa zamani pia wamesisitiza kwamba halengi kurejea madarakani, ila kuchangia katika mstakabali wa utawala bora nchini DRC pamoja na hali ya usalama mashariki  nchi hiyo.

Licha ya Rais Kabila kuondolewa kinga ya kutoshtakiwa ameapa kushiriki kwenye mazungumzo ya kutafuta suluhu kwa matatizo yanayokumbwa taifa lake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii