Mpango wa London kupunguza misaada ya nje kutaathiri baadhi ya nchi za Afrika

Mpango wowote wa chama cha Labour nchini Uingereza Kupunguza misaada ya nje kutaathiri elimu ya watoto na kuongeza hatari ya magonjwa na vifo katika baadhi ya nchi za Afrika, hii ni kulingana na tathmini ya ndani iliyofanywa na serikali.

Serikali ya Waziri Mkuu Keir Starmer, mapema mwaka huu ilitangaza kuwa itapunguza bajeti yake inayoelekezwa katika misaada kutoka asilimia 0.5 hadi 0.3 kama njia moja ya kuziba pengo linalotokana na matumizi yake ya ulinzi.

Tayari London imeanza kupunguza ufadhili wake katika bajeti ya mwaka wa 2025- 2026, mataifa 11 ambayo yamekuwa yakinufaika katika vita dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika yakitarajiwa kuathirika.

Mataifa hayo ni pamija na DRCMsumbijiZimbabwe na Ethiopia ambayo yamekuwa yakinufaika na msaada ya Uingereza katika masuala ya afya ya wanawake na utayari wa kukabiliana na majanga ya dharura.

Sekta ya elimu katika nchi za EthiopiaSierra LeoneNigeria na Zimbabwe pia zitaathirika.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii