VITUO VYA KUPUNGUZA KASI YA MAFUTA KUJENGWA

Jumla ya vituo viwili vya kupunguza kasi ya mafuta ghafi yanayotoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani- Tanga, vinatarajia kujengwa ili kusaidia upunguzaji wa kasi ya mafuta ghafi yanayosafirishwa sambamba na kulinda miundombinu ya bomba hilo la mafuta.
Hayo yamesemwa na Mtaalam wa Ujenzi wa Miundombinu hiyo kutoka kituo namba moja (PRS-1) inayojengwa Kata ya Kibaya, Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara Mhandisi Damian Lasway, wakati alipokuwa akizungumzia maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya kituo hicho ambapo amesema ujenzi wa kituo umefikia asilimia 50.
Amesema ujenzi wa vituo hivyo utaenda sambamba na wa nchini Uganda, ambapo kwa hapa nchini vituo hivyo viwili vitajengwa sambamba na vile vya kusukuma mafuta vitakavyojengwa Muleba, Mbogwe, Igunga na Singida na vingine viwili vitakuwa nchini Uganda.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii