Dira ya taifa nyonzo muhimu kujua wajibu wetu

Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewataka Watanzania kuipokea kwa matumaini Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025–2050, akisema inaakisi kwa kina dhamira ya kuleta ustawi wa maisha ya wananchi na maendeleo jumuishi ya Taifa.

Dk. Mwinyi amesema hayo leo Alhamisi, Julai 17, 2025, katika hafla ya uzinduzi wa dira hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, ambapo mgeni rasmi ni Rais Samia Suluhu Hassan.

“Hakika leo ni siku muhimu na ya kihistoria ambapo nchi yetu inafungua ukurasa mpya kwa kuzindua dira mpya inayotoa mwelekeo wa maendeleo ya Watanzania katika kipindi cha miaka 25 ijayo,” amesema Dk Mwinyi na kuongeza kuwa dira hiyo ni nyenzo muhimu kwa Taifa, itakayotumika kuelekeza mipango na hatua mbalimbali za maendeleo kwa muda mrefu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii