TARURA imetoa mafunzo kwa watumishi wapya 98

WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imetoa mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo watumishi wapya 98 wa Kada ya Uhandisi, Fundi Sanifu, Maofisa Hesabu, Wachumi pamoja na Ununuzi na Ugavi.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Jiji, katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma yakiongozwa na Mkurugenzi wa Huduma Saidizi wa Tarura, Azimina Mbilinyi akishirikiana na Idara nyingine TARURA Makao Makuu.

Aidha, mafunzo hayo yaliwataka watumishi hao wapya kufanya kazi kwa weledi na ufanisi na kufuata maadili ya utumishi wa umma wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.

Katika mafunzo hayo mada mbalimbali zilitolewa kwa watumishi hao ikiwemo kuhusu sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma ambapo pia walikula viapo vya uadilifu wa utumishi wa umma kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii