Mchakato wa kuwapata wabunge viti maalumu kwa mkoa wa Lindi umetamatika baada ya mtangazaji wa Clouds Media, Kijakazi Yunus kushinda kwa kura nyingi huku akiwabwaga wakongwe.
Akitangaza msimamizi wa uchaguzi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara , Kanal Patric Sawalla amesema kuwa Kijakazi Yunus amepata kura 942 huku Zainab Kawawa amepata kura 492.
“Washindi wetu wa ubunge viti maalum kwa Mkoa wa Lindi ni Kijakazi Yunusi pamoja na Zainabu Kawawa.”amesema Kanal Sawalla
Kwa upande wake Kijakazi Yunus akizungumza baada ya matokeo hayo, amewashukuru wanawake wa mkoa wa Lindi kwa kuweza kumpa kura nyingi huku akiwaahidi ushirikiano ulitukuka.
“Nimegombea hii ni mara ya tatu niwaombe wanawake wenzangu na vijana hatupaswi kukata tamaa ushindi huu ni wetu sote niwahidi ushirikiano ili tuweze kuleta maendeleo katika mkoa wetu wa Lindi.”amesema