Mahakama ya Wilaya ya Pangani mkoani Tanga imemhukumu kifungo cha miaka 20 jela, Idd Shelugwaza (26) ambaye ni mkulima na mkazi wa Kijiji cha Kwakibuyu, baada ya kukutwa na hatia ya kosa la shambulio la aibu dhidi ya mtoto mwenye umri wa miaka minne.
Tukio hilo lilitokea Juni 24,2025 katika Kijiji cha Kwakibuyu, ambapo Idd Shelugwaza alitenda kosa hilo dhidi ya mtoto ambaye ni mwanafunzi na mkazi wa kijiji hicho.
Hakimu Francisca Magwiza, akisoma hukumu hiyo, ameeleza kuwa mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, na hivyo kumkuta mtuhumiwa na hatia ya shambulio la aibu.
Amesema mtuhumiwa amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela ili kutoa fundisho kwa jamii na kulinda haki za watoto.