Machafuko Colombia yaua 18 na majeruhi 40

NCHINI  Colombia , watu 18 wamefariki  dunia na wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa baada ya kushambuliwa na kundi la waasi.

Akizungumzia kuhusu tukio hilo nchini Colombia, Rais Gustavo Petro amesema makundi yaliyokataa makubaliano ya amani ya mwaka 2016 ndiyo yanayohusika.

Katika mji wa Cali, gari lililobeba vilipuzi lililipuka karibu na kambi ya jeshi la anga na kuua watu sita huku 71 wakijeruhiwa.

Hapo awali, helikopta ya polisi ilidunguliwa kwenye eneo la Amalfi na kuua maafisa 12.

Rais Gustavo Petro amesema makundi yaliyokataa makubaliano ya amani ya 2016 ndiyo yanahusika. 

Machafuko hayo yamekuwa yakiendelea kwa miongo kadhaa na kusababisha vifo vya zaidi ya nusu milioni.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii