WHO kuripoti tukio la joto kazini tishio kwa afya ulimwenguni

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) wamesema mamilioni ya wafanyakazi  dunia wamekuwa wanakumbana na hali ya joto kali wakiwa makazini na kuahatrisha afya zao .

Ripoti hiyo imeziomba mamlaka mbalimbali za serikali , waajiri na wafanyakazi duniani kushirikiana kuandaa mikakati madhubuti ya kukabiliana na tatizo hilo.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza tangu 1969 kwa WHO kutoa ripoti mahsusi kuhusu joto kazini.

Mkurugenzi wa mazingira na afya wa WHO, RĂ¼diger Krech, amesema ugunduzi wa ripoti hiyo unatoa muongozo wa dunia kuanza kuchukua hatua kudhibti athari za mabadiliko ya tabianchi .


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii