Marais watatu waungana kupinga matendo ya serikali iliyopo madarakani

Marais watatu wastaafu nchini Somalia Sharif Sheikh Ahmed, Abdiqasim Salad Hassan na Mohamed Abdullahi Farmaajo wameungana kutoa tamko dhidi ya Serikali ya Rais Hassan Sheikh Mohamud, wakiilaani kwa uporaji na uuzaji holela wa ardhi ya umma bila kuzingatia taratibu za Kisheria na usimamizi unaostahili.

Viongozi hao wamesema Serikali imekuwa ikihamisha umiliki wa ardhi bila kuhusisha Mamlaka ya Mikataba ya Taifa, na kutoingiza mapato kwenye Hazina ya Taifa. Hali inayosababisha Wananchi maskini wa Mogadishu kufukuzwa na kuondolewa katika makazi yao.

Wametaka Wananchi na Wafanyabiashara kuepuka kununua au kushiriki katika mali zilizopatikana kwa njia zisizo halali, wakisema ni mikataba hatarishi na isiyo na uhalali, hatua ambayo imepongezwa na makundi ya uharakati.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii