Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limewakamata madereva wa tano wa magari yanayosafirishwa njeya Nchi (IT) kwa makosa ya kusafirisha abiria bila kibali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa Waandishi wa Habari na Kamanda wa Polisi Mkoaa wa Morogoro SACP Alex Mkama, imeeleza kuwa ukamataji huo umefanyika usiku wa Agosti 20, 2025 katika eneo la Mikumi Wilaya ya kipolisi Ruhembe katika operesheni maalum inayolenga kudhibiti usalama wa watumiaji wa barabara.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa waliokamatwa ni Richard George Kunambi (40) Dereva na Mkazi wa Dar es salaam aliyekuwa ikiendesha Gari namba IT. 7543 Toyota Probox, Shabani Ricard Nwambuli (37) mkazi wa Mbeya aliyekuwa akiendesha gari namba IT. 3040 Mercedes Benz, Mstapaha Said Kikombe (39) Mkazi wa Dar es salaam aliyekuwa akiendesha gari namba IT.1682 Toyota Parado.
Omary Mohammed Mwinjega (40) Dereva na Mkazi wa Dar es salaam aliyekuwa na gari namba IT. 1100 AINA YA Nissan Extail na Ambwene Benson Kipenya (44) Dereva na MKazi wa Dar es salaam aliykuwa akiendesha gari namba IT. 5527 Toyota Sienta.
Madereva waliokamatwa watafaikishwa kwenye vyombo vingine vya haki jinai ili kukamilisha mchakato wa upatikanaji wa haki huku Jeshi hilo likiwataka madereva wanaosafirisha magari kwenda nchi za nje kuacha tabia hiyo kwa magari hayo hayana usajili wa kusafirisha abiria, wenye kukaidi katazo hilo kuchukuliwa hatua kwa maujibu wa sheria.