Zaidi ya washiriki 500 na wengine 100 kutoka nchi za nje wanatarajiwa kushiriki maonesho ya 20 ya Biashara kwa lengo la kufungua fursa kwa wafanyabiashara wa kada zote Afrika mashariki, yatakayofanyika katika viwanja vya Nyamagana mkoani Mwanza.
Maonesho hayo yataratibiwa na Taasisi ya Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Mwanza ambayo yatafanyika tarehe 29 Agosti hadi 7 Septemba 2025 na yatafuguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa Mwanza, Said Mtanda.
Washiriki wanaotarajiwa kuhudhuria maonesho hayo ni 500 na wengine 100 kutoka mataifa mabalimabli ambapo yakitarajiwa kufikia watembeleaji 250,000 kutoka ndani na nje ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza, Gabriel Kenene amesema yatafungua fursa kwa wafanyabiashara, wakulima, wenye viwanda,na wajasiliamali ili waweze kujulikana na kutanganza bidhaa zao.
Kanene amesema kutakuwa na bidhaa za mashine na teknolojia, Bidhaa za ujenzi thamani za nyumbani na ofisini, bidhaa za kilimo na mifugo, Bidhaa za usindikaji na vinywaji Bidhaa za hoteli na utalii, sanaa na kazi za mikono,bidhaa za mawasiliano ya habari.