Makalla aapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan leo August 26 mwaka huu Ikulu Jijini Dodoma amemuapisha CPA Amos Gabriel Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Kabla ya hivi karibuni kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Makalla amewahi pia kuwa Mkuu wa Mikoa wa Mbeya, Dar es salaam na Mwanza kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii