Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Wilaya ya Ilemela kwa umbali wa zaidi ya kilometa 48.8, ambapo utazindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi 9 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 27.6.
Akizungumza wakati wa mapokezi ya Mwenge huo kutoka Wilaya ya Nyamagana katika uwanja wa furahisha , Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe. Amir Mkalipa, amewataka wananchi wa Ilemela kujitokeza kwa wingi kushiriki katika miradi itakayozinduliwa na Mwenge huo.
Aidha Mkalipa amesema kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani humo, kutakuwa na shughuli za upimaji afya kwa wananchi watakaojitokeza kwenye mkesha utakaofanyika katika viwanja vya Nyamhongolo.
Mwenge wa Uhuru mwaka huu unakimbizwa ukiwa na kauli mbiu isemayo:
“JITOKEZE KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 KWA AMANI NA UTULIVU”,
ikiwahamasisha wananchi kujitokeza kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye october mwaka huu kwa Aman na Utulivu.