Marekani imetangaza kuwa inaifuatilia Venezuela kwa lengo la kuikamata meli nyingine ya mafuta inayodai kutumiwa na serikali yake kukwepa vikwazo vya biashara ya mafuta vilivyowekwa na Washington.
Katika taarifa iliyotolewa na walinzi wa pwani wa Marekani wamesema kuwa meli hiyo inayosafiri kwenye bahari ya Karibia inapeperusha bendera ya uongo na ni miongoni mwa meli za mafuta zilizo chini ya vikwazo vya Marekani.
Aidha iwapo wataikamata Meli hiyo itakuwa meli ya tatu yenye mafungamano na biashara ya mafuta ya Venezuala -- taifa ambalo Washington inalituhumu kufadhili biashara ya dawa za kulevya.
Hata hivyo hapo desemba 21 mwaka huu walinzi hao wa pwani waliikamata meli nyingine wanayoituhumu kusafirisha mafuta ya Venezuela,ikiwa ni wiki mbili tangu walipoizuia meli nyingine ambapo serikali ya Rais Nicolas Maduro wa Venezuela imezitaja hatua hizo za Marekani kuwa "wizi na uharamia" wa kimataifa.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime