Wananchi wa kata ya Nyakato mtaa wa NHC, uliopo wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, wameishukuru Serikali kwa kuwajengea jengo jipya la mama na mtoto katika zahanati ya Nyakato.
Wakizungumza na Jembe Habari wananchi hao wamesema jengo hilo litakuwa mkombozi kwao, kwani awali walilazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma katika kituo cha afya Buzuruga.
Wameeleza kuwa jengo hilo ni la kisasa, lina vifaa vya kutosha na litawawezesha akinamama kujifungua salama.
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Fredrick Mtiba, amesema ujenzi wa mradi huo umepunguza msongamano wa wagonjwa katika kituo cha afya Buzuruga, hali iliyosaidia ongezeko la utoaji wa huduma bora.
Akizindua rasmi jengo hilo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Ismail Ussi, ameipongeza Serikali kwa kukamilisha ujenzi wa zahanati katika viwango vinavyotakiwa.
Aidha, Ussi amewataka wananchi kutunza miundombinu ya jengo hilo kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Wananchi wa kata ya Nyakato mtaa wa NHC, uliopo wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, wameishukuru Serikali kwa kuwajengea jengo jipya la mama na mtoto katika zahanati ya Nyakato.
Wakizungumza na Jembe Habari wananchi hao wamesema jengo hilo litakuwa mkombozi kwao, kwani awali walilazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma katika kituo cha afya Buzuruga.
Wameeleza kuwa jengo hilo ni la kisasa, lina vifaa vya kutosha na litawawezesha akinamama kujifungua salama.
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Fredrick Mtiba, amesema ujenzi wa mradi huo umepunguza msongamano wa wagonjwa katika kituo cha afya Buzuruga, hali iliyosaidia ongezeko la utoaji wa huduma bora.
Akizindua rasmi jengo hilo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Ismail Ussi, ameipongeza Serikali kwa kukamilisha ujenzi wa zahanati katika viwango vinavyotakiwa.
Aidha, Ussi amewataka wananchi kutunza miundombinu ya jengo hilo kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo