Mapafu ya nguruwe yatumika kupandikizwa binadamu

MADAKTARI Bingwa nchini China wamefanikiwa kupandikiza mapafu kutoka kwa nguruwe kwenda kwa binadamu. Kwa mujibu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Njia ya Hewa ya mjini Guangzhou umeonyesha kuwa mapafu hayo yalifanya kazi  kwa mgonjwa ambaye ubongo wake ulikuwa haufanyi kazi na yakamsaidia kupumua kwa siku tisa bila matatizo

Wanasayansi hao wamesema utafiti huo ni hatua kubwa katika kukabiliana na uhaba wa viungo vya upandikizaji duniani, ingawa bado kuna changamoto kubwa kutokana na uchangamano wa mapafu na hatari ya maambukizi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii