Urusi imeahidi kujenga kituo cha umeme wa nyuklia

SERIKALI ya Urusi imeahidi kujenga kituo cha umeme wa nyuklia nchini Niger, taifa linaloongoza kwa urani barani Afrika lakini likitegemea umeme kutoka nje.

Kampuni ya Serikali ya Rosatom imesaini makubaliano ya kushirikiana kwenye nishati na kutoa mafunzo kwa wataalamu wa Niger. Hatahivyo  taarifa zinasema kuwa utekelezaji wa mradi huo utakuwa mradi wa kwanza kutekelezwa Afrika Magharibi.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wamedai kuwa hatua hiyo itaongeza ushawishi wa Moscow Barani Afrika, hasa baada ya Niger kutofautiana na Ufaransa

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii