DRC, Rwanda zakubaliana kurejesha wakimbizi

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi (UNHCR) limesema DRC na Rwanda zimekubaliana kuwarejesha makwao wakimbizi walioathiriwa na machafuko Mashariki mwa Congo.

Mkuu wa UNHCR, Filippo Grandi, amesema zaidi ya wakimbizi 500 wa Rwanda walirudishwa makwao siku mbili zilizopita. Amesema zoezi hilo lazima lifanyike kwa hiari, huku mashirika ya haki za binadamu yakiendelea kushutumu kundi la M23 kwa kuwafukuza raia. 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii