Wawili wauawa na zaidi ya mia moja watekwa nyara Zamfara

Watu wenye silaha wamewauwa takriban watu wawili na kuwateka nyara zaidi ya watu 100, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, katika shambulio lililotokea katika Jimbo la Zamfara, Nigeria, maafisa wa eneo hilo na viongozi wa kijamii wamesema.


Huzaifa Isa, mkazi wa Gamdum Mallam, amesema washambuliaji waligawanyika katika makundi mawili. "Kundi moja liliteka nyara watu na mifugo, huku liingine likiweka kizuizi kwenye lango kuu la Adafka, likimpiga risasi mtu yeyote aliyejaribu kuvuka," amesema. "Tulitendewa kama watumwa kwenye ardhi yetu, kana kwamba hakuna serikali."

Mbunge wa eneo hilo Hamisu Faru alithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa njia ya simu. "Takriban watu 100 wametekwa nyara tangu siku ya Jumamosi asubuhi," ameongeza. "Majambazi hao walishambulia Nasarawa Burkullum wakati mvua iliyokuwa ikinyesha, wakavuka mto hadi vijiji jirani, na kuwateka nyara watu wengine 46 katika kijiji cha Ruwan Rana."

Wakaazi wanahofia mashambulizi zaidi huku kundi hilo lenye silaha likiripotiwa kujaribu kuvuka tena mpaka wa msitu

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii