Constant Mutamba kufungwa miaka 13 jela

Kesi hiyo, iliyoanza mwezi mmoja uliopita dhidi ya aliyekuwa Waziri wa Sheria wa Kongo Constant Mutamba, anayetuhumiwa kujaribu kutakatisha karibu dola milioni 20, imefungwa siku ya Jumatano, Agosti 13, 2025. Mwendesha mashtaka ameomba miaka 10 ya kazi ya kulazimishwa, huku upande wa utetezi ukiamini kuwa hakuna uhalali wa kumtia hatiani Constant Mutamba, ambaye anajulikana kwa kurekebisha makosa yake na kimahakama ambayo yalimuweka katika mutano mkubwa na majaji kwa miezi kadhaa.

Mbali na miaka 10 ya kazi ya kulazimishwa, mwendesha mashtaka ameongeza muongo mwingine wa kutoshikilia wadhifa wowote rasmi baada ya kutumikia kifungo chake. Hatua hii imezua hasira ya mwendesha mashtaka dhidi ya Constant Mutamba, ambaye ametajwa hadharani kuwa "mkosaji." Alikuwa amejiruhusu, mwendesha mashitaka anakumbusha, "kuinajisi mahakama kwa kufanya mikutano ya hadhara." Alidai kuwa uhamisho wa karibu dola milioni 20 (takriban Euro milioni 17) ulikuwa umefanywa kwa kandarasi isiyo ya kawaida ya umma, iliyotolewa kwa "kampuni hewa."

Upande wa utetezi umedai kuwa hakuna dola hata moja iliyofujwa kuhusiana na kandarasi yenye utata ya ujenzi gereza huko Kisangani, kaskazini mashariki mwa DRC. Kwa mujibu wa upande wa utetezi, kunakili kwa waziri huyo wa zamani amri ya malipo kwa Mkaguzi Mkuu wa Fedha na vyombo vingine vya uangalizi kufuatilia mienendo ya fedha zilizohamishiwa kwenye akaunti ya kampuni ya ujenzi ni uthibitisho wa imani nzuri ya Constant Mutamba.

Kwa upande wake, amebaini kwamba taratibu za kisheria zilikuwa na lengo moja tu: kumwondoa serikalini. Uamuzi wa Mahakama Kuu utatolewa baada ya wiki mbili, tarehe 27 Agosti.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii