Watu kadhaa wauawa katika mashambulizi dhidi ya wanaounga mkono jeshi Al-Jazeera

Shambulizi la ndege zisizo na rubani limelenga mji wa Tambul, kusini mashariki mwa Khartoum, siku ya Jumatano, Agosti 13, 2025, wakati sherehe za jeshi zilikuwa zikiendelea. Tambul iko katika Jimbo la Al-Jazeera, ambalo limerejea katika hali yake ya kawaida tangu jeshi lilipolirejesha kwenye himaya yake mnamo mwezi Machi 2025.

Ulinzi wa anga wa kikosi cha "Al-Jazeera Shield" uliamilishwa kujibu shambulio hilo, mkazi wa mji huo amesema, akielezea "hali ya machafuko" katika uwanja wa kati ambapo "mamia ya watu walikuwa wamekusanyika." Kwa mujibu wa mashahidi, watu wawili waliuawa na dazeni kujeruhiwa. Makombora yaliyotumiwa kwa sasa yanachnguzwa ili kubaini asili yao na waliohusika na shambulio hilo.

Hili ni shambulio la kwanza kukumba eneo hili lenye utulivu tangu mwezi Machi 2025. Mashambulizi hayo yalilenga vikosi vya Al-Jazeera Shield, vikiongozwa na Abu Akla Kikel, ambavyo vinachukuliwa kama msaidizi wa jeshi.

Kulingana na duru za Al-Jazeera, Jenerali Kikel ndiye aliyelengwa, lakini hakuna taarifa zozote kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwake katika sherehe za kuadhimisha miaka 71 tangu kuanzishwa kwa jeshi la Sudan. Jenerali Kikel, anayetoka katika jimbo la Al-Jazeera, alitoa taarifa zilizorekodiwa kufuatia mashambulizi hayo. Alitangaza kuwa vikosi vyake vinajiandaa kuelekea Kordofan na Darfur kusaidia jeshi katika maeneo hayo.

"Al-Jazeera Shield ina adui mmoja tu, na huyo ni wanamgambo wa familia ya Daglo," alitangaza. Al-Jazeera Shield na Kikel walijitoa kwa wanamgambo wa RSF kabla ya kujiunga na jeshi mnamo mwezi Oktoba 2024. Vikosi hivi vilihusika pakubwa kwa jeshi kuliwka tena kwenye himaya yake jimbo la al-Jazeera.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii