Vikosi vya uokoaji vimefanikiwa kuokoa Wachimbaji wanne kati ya 25 wafukiwa na kifusi Agost 11 Mwaka huu wakati watengenza Maduara katika Mgodi mdogo wa Nyandolwa unaomilikiwa na kikundi cha Wachapakazi mkoani Shinyanga huku mmoja kati ya hao akifariki dunia wakati apatiwa matibabu.
Kwa Mujibu wa taarifa iliyolewa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro,amesema aliyefariki dunia ni Emmanuel Kija(20-25),na ambaye amepewa rufaa kwenda katika hospitali ya Bugando ni Fulano Peter (27) na ambao afya zao zimeimarika na kuruhusiwa na Athony Clement na Nigula Japhet.
Leticia Ndege , Michael Petro na Catherine Jastine ni miongono mwa watu ambao ndugu zao wamefukiwa na mgodi huo wameiba serikali kuongeza nguvu huku Naibu waziri wa Madini Stephen Kiruswa akitoa kauli ya serikali.