Wakazi wa kijiji cha Majimbo, kaunti ya Embu, waliachwa na butwaa baada ya kugunduliwa kwa miili ya wanawake wawili wasiojulikana kwenye kijito.
wakazi wa eneo la Dallas walikumbana na miili miwili iliyooza ya wanawake wachanga iliyotupwa kando na Kanisa la Deliverance katika Mto Matakari. Wakazi waliokuwa na mshtuko walikusanyika eneo la tukio baada ya habari za ugunduzi huo wa kutisha kusambaa. Waathiriwa, ambao majina yao hayajatambulika, walionekana kwa mara ya kwanza na wakazi wa eneo hilo waliokimbilia kuwajulisha maafisa wa usalama. Polisi waliofika walipiga kizuizi eneo hilo na kuanzisha uchunguzi wa mauaji yanayoshukiwa kutokea.
Mita chache kutoka eneo lilipogunduliwa miili hiyo, kulikuwa na jengo dogo linalofanana na nyumba, lakini wakazi wenye hasira waliiteketeza kwa moto.