Afisa wa Ngazi ya Juu Afutwa Kazi, Atuhumiwa Kumteka Nyara Mwanahabari Aliyefichua Ufisadi

Utawala wa Gavana Gladys Wanga umemchukulia hatua afisa mkuu anayedaiwa kumpiga mwanahabari.

Katika taarifa kwa vyumba vya habari mnamo Jumatatu, Septemba 14, kaunti ilitangaza kuzuiwa kwa Beatrice Mercy Akugo, afisa wa rasilimali watu.

“Serikali ya kaunti leo, kuanzia sasa, imechukua hatua madhubuti kumzuia Bi Beatric Mercy Akugo, Afisa wa Rasilimali Watu, katika Idara ya Barabara, Uchukuzi na Kazi za Umma.

"Uamuzi huu unafuatia shtaka kubwa kwamba Akugo anakabiliwa na madai ya kuhusika katika utekaji nyara, shambulio na vitisho kwa mwanahabari. Maelezo yanayodaiwa kuhusu tukio hilo ni ya kuchukiza na ni pamoja na mwanahabari huyo kutekwa nyara, kushikiliwa kinyume na matakwa yake, kushambuliwa kimwili na kutishiwa," Atieno Otieno, msemaji wa kaunti alisema.

Otieno alisema kuwa kuzuiwa ni utaratibu wa kawaida ambao ungeruhusu uchunguzi usio na upendeleo katika madai dhidi ya Akugo

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii