Ameir kila Mzanzibar atalipwa Tsh 500,000 kwa mwezi

Mtiania urais wa Zanzibar kupitia Chama Demokrasia Makini, Ameir Hassan Ameir (kushoto), amesema iwapo atapitishwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na kupata ridhaa ya wananchi kuwa Rais, kila Mzanzibari atalipwa Sh500,000 kwa mwezi ili kuondoa daraja lililopo la wenye nacho, kwa kuwa wengine hawana badala yake wanaishi maisha ya kubahatisha.

Ameir amesema hayo leo Septemba mosi, 2025 wakati akipokea mkoba wenye fomu za urais kutoka kwa Mwenyekiti wa ZEC, Jaji George Joseph Kazi katika ofisi za tume hiyo, Maisara Unguja Zanzibar. 


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii