Wapiga kura wanasubiri matokeo ya uchaguzi mkuu wa urais

Raia wa Malawi wanasubiri matekeo ya uchaguzi wa urais, baada ya kushiriki uchaguzi Jumanne kuwachagua viongozi wao.

Mbali metekeo ya urais raia hao pia wanasubiri matekeo ya wabunge na madiwani, wagombea wakuu ambao rais wa sasa Lazarus Chakwera na rais wa zamani Peter Mutharika, wote wamekuwa wakinadi sera zao kwa misingi ya kuimarisha uchumi wa Malawi ambao umekuwa ukiyumba, iwapo watachaguliwa, japo kuna wagombea wengine 15, akiwemo pia rais wa zamani Joyce Banda.

Iwapo viongozi hao wawili hawatafikisha asilimia 50 ya kura zote zilizopingwa basi duru ya pili ya kura itafanyika ikiwashirikiasha Chakwera na Mutharika, tume ya uchaguzi ina hadi Septemba 24 kutangaza matekeo rasmi ya uchaguzi huo, kwa mjibu wa sheria.

Nchi ya malawi ni moja ya nchi maskini zaidi duniani kwa muda sasa, na kuongezeka kwa gharama ya maisha nchini humo, kumechangia ukosefu wa sarafu za kigeni.

Kwa muda sasa nchi hiyo imekuwa ikishuhudia ukosefu wa nguvu za umeme na mafuta, vijana nao wakiendelea kutuhumu serikali ya rais Chakwera kwa kukosa kubuni nafasi za ajira.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii