Uingereza na Ureno kutambua rasmi taifa la Palestina

Licha ya shinikizo kali kutoka kwa Marekani na Israel, na bila ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lenye hadhi ya juu, Uingereza na Ureno zitalitambua rasmi taifa la Palestina leo Jumapili.

Uingereza na Ureno zinajiandaa kulitambua rasmi taifa la Palestina leo Jumapili, licha ya shinikizo kali kutoka kwa Marekani na Israel.

Uamuzi huu unakuja katika mkesha wa kufunguliwa kwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kuashiria mabadiliko ya kidiplomasia kwa London, ambayo kwa muda mrefu ilichukuliwa kuwa mshirika mkubwa wa Israel.

Kwa miezi kadhaa, idadi inayoongezeka ya nchi za Magharibi zimechagua kuchukua hatua hii, kujibu kuongezeka kwa hujuma ya Israel huko Gaza, iliyochochewa na shambulio kuu la Hamas mnamo Oktoba 2023.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii