Rais Dina Boluarte atimuliwa mamlakani na Bunge

Rais wa Peru Dina Boluarte ametimuliwa usiku wa Alhamisi, Oktoba 9, kuamkia Ijumaa, Oktoba 10, kwa kura nyingi za wabugne, kufuatia hoja kadhaa zilizowasilishwa wakati wa mchana na makundi mbalimbali ya vyama vya siasa bungeni.

"Kutimuliwa kwa rais kumeidhinishwa," ametangaza Spika wa Bunge José Jerí, kufuatia kikao kifupi ambacho Boluarte hakufika, licha ya kutakiwa kushiriki. Boluarte anaweza kujitetea au kuwakilishwa na wakili, amesema Spika wa Bunge José Jerí.

Kwa kumtimua madarakani, angalau wabunge 87 kati ya 122 walioshiriki katika kura hiyo walilazimika kupiga kura kuunga mkono kuondolewa kwake madarakani. Vyama vikuu vya kisiasa katika Bunge viliwasilisha hoja tano za kumtimua madarakani wakati wa mchana. Uchunguzi wa hoja nne kati hizo zilipitishwa kwa kura nyingi katika Bunge la nchi hiyo.

Hoja hizo zinahimiza "kutokuwa na uwezo wa kudumu wa maadili" wa rais kutekeleza majukumu yake, kulingana na hati zilizosomwa wakati wa ufunguzi wa kikao cha bunge. Dina Boluarte tayari amekuwa mlengwa wa majaribio kadhaa ya kumfungulia mashtaka, ambayo hakuna hata moja lililofanikiwa. Wakati huu, mchakato huo umefikia hitimisho lake, huku vyama vya mrengo wa kulia na vyamav yenye msimamo mkali vya mrengo wa kulia  ambavyo hapo awali vilimuunga mkono vikimtelekeza.

Kukosekana kwa utulivu wa kisiasa

Peru inakabiliwa na kipindi kibaya zaidi cha machafuko ya kisiasa katika historia yake ya kisasa, baada ya kuongozwa na marais sita katika takriban miaka tisa. Baada ya kuingia madarakani baada ya kufutwa kazi kwa Rais Pedro Castillo, huku kukiwa na maandamano yaliyokandamizwa kwa nguvu na kusababisha vifo vya takriban watu 50, Dina Boluarte anakabiliwa na hali ya kutopendwa na watu wengi.

Muhula wake pia umekumbwa na kashfa kadhaa, ikiwa ni pamoja na kashfa ya "Rolexgate", inayohusisha saa za kifahari na vito alizodaiwa kushindwa kutangaza, hali iliyoshuhudiwa mnamo mwezi Julai 2023 ambayo ulifanywa kuwa siri licha ya sheria kumtaka aarifu Bunge.

Katika wiki za hivi karibuni, maandamano dhidi ya serikali yaliongezeka huko Lima huku kukiwa na wimbi la unyang'anyi na mauaji yaliyohusishwa na uhalifu uliopangwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii