MKAKATI SHIRIKISHI KUANZISHWA ILI KUPAMBANA NA CHANGAMOTO YA UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Balozi Dkat. Batilda Burian amewataka Viongozi wa Vijiji na Kata kwa kushirikiana na Viongozi wa Wilaya kuhakikisha wanaweka misingi madhubuti ya kiusalama katika kusimamia na kulinda vyanzo vya maji hususan kwa kudhibiti shughuli za uchimbaji wa madini zinazoendelea katika maeneo ya chanzo cha maji cha Mto Zigi.

Balozi Batilda ametoa wito huo wakati wa ziara yake akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa iliyotembelea na kukagua eneo la chanzo cha maji cha Mto Zigi ambacho kimeathiriwa na shughuli za kibinadamu Balozi Batilda ametoa onyo kali kwa watu wote wanaojihusisha na uchimbaji wa madini katika maeneo ya vyanzo vya maji vya Mto Zigi na maeneo mengine ndani ya Mkoa wa Tanga.

Pamoja na hayo pia amewataka viongozi wa ngazi zote kuunda mkakati shirikishi unaolenga kupambana na uharibifu wa vyanzo vya pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu fursa mbadala za kiuchumi, hasa katika sekta ya kilimo ili kuwasaidia kuachana na shughuli haramu zinazochangia uharibifu mkubwa wa mazingira.

Awalia akitoa taarifa ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TangaUWASA Dkt. Fungo Ali Fungo amesema kuwa pamoja na jitihada kubwa zinazoendelea katika uhifadhi wa vyanzo vya maji kwa kushirikiana na Umoja wa Wakulima Wahifadhi Mazingira Kihuwhi Zigi (UWAMAKIZI) bado changamoto kubwa inayowasumbua ni shughuli za uchimbaji wa madini kwenye vyanzo vya maji jambo ambalo linahatarisha uwepo wa maji ya kutosha na hivyo kuiomba serikali kuingilia kati ili kuwezesha uhakika wa upatikanaji wa maji ya kutosha.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii