Vyombo vya habari vinakabiliwa na shinikizo kutoka kwa mamlaka

Nchini Mali, wakati wa miaka mitano ya Mpito, uhuru wa raia umepunguzwa kwa kiasi kikubwa. Vyama vya siasa vimevunjwa, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii vinafuatiliwa kwa karibu, na kesi za kisheria na kiutawala dhidi ya wakosoaji wa mamlaka ni nyingi kupita kiasi.

Kwa zaidi ya miezi miwili, mashambulizi ya wanajihadi yamekuwa yakiongezeka, na nchi inakabiliwa na uhaba wa mafuta uliosababishwa na JNIM, kundi linalodai kuunga mkono Uislamu na Waislamu, mshirika wa Al Qaeda. Vyombo kadhaa vya habari viliwekewa vikwazo katika siku za hivi karibuni.

Nchini Mali, baada ya wakurugenzi wake kuitwa Jumanne, Novemba 18, na HAC (Mamlaka Kuu ya Mawasiliano), kituo cha Runinga cha Joliba bado kinasubiri uamuzi kuhusu hatima yake. Sababu: ripoti kuhusu kutoroka kwa wakazi wa Loulouni kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na wanajihadi wa JNIM. Baada ya wanajihadi kuondoka, vikosi vya Mali viliujresha mji huo kwenye himaya yake. Kituo hicho pia kilitangaza ripoti kuhusu kuwasili kwa wanajeshi wa Mali huko Loulouni.

Joliba TV ilisimamishwa mwaka mmoja uliopita, mnamo Novemba 2024, kwa miezi sita, baada ya kurusha mjadala unaohoji ukweli wa mapinduzi yaliyodaiwa kuzuiwa nchini Burkina Faso.

Vituo vitatu vya redio vyasimamishwa

Vituo vitatu vya redio vya ndani tayari vimesitisha matangazo yao, baada ya kusimamishwa Novemba 13, wiki iliyopita, kwa miezi mitatu.

Redio Aadar Koïma huko Gao ilichukuliwa vikwazo kwa kukosoa, katika taarifa ya habari iliyorushwa Novemba 4, tabia ya baadhi ya askari wakati wa doria za usiku, ikiwatuhumu kwa kushirikiana na wezi wa dukani. Mamlaka Kuu ya Mawasiliano (HAC) inaona kuwa hili "dharau na ni tusi kubwa" dhidi ya jeshi

Redio Aadar Koukia ya Ansongo, kwa upande wake, iliripoti mnamo Novemba 2 kuwepo kwa harakati za maandamano dhidi ya mamlaka ya mpito. Haya yalikuwa "madai yasiyo na msingi" ambayo yanaweza kuhatarisha "utaratibu wa umma," kulingana na mamlaka ya mawasiliano.

Mwanzoni mwa mwezi, waandishi wa habari wawili kutoka vituo hivi vya redio walikamatwa na polisi na kuzuiliwa kwa muda kwa sababu hizo hizo.

Waziri Abdoulaye Diop, chanzo cha mgogoro

Kikwazo kama hicho, kusimamishwa kwa miezi mitatu, kilichukuliwa dhidi ya Radio Kayira huko Kolondieba, mkoa wa Sikasso. Kituo hiki cha redio ni cha mtandao ulioanzishwa na chama cha siasa cha Sadi cha kiongozi wa upinzani aliye uhamishoni Oumar Mariko. Utata huo unatokana na matangazo ya Oktoba 26 ambapo matamshi yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje yalijadiliwa. Abdoulaye Diop alisema kwamba Modibo Keïta, rais wa kwanza wa Mali huru, alikuwa "mwalimu wa shule" ambaye "hakuwa amejiandaa kuongoza nchi." Akikabiliwa na wimbi la hasira lililofuata, waziri huyo alibatilisha kauli zake katika ujumbe uliochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, maoni yaliyotolewa na mwandishi wa habari na wasikilizaji waliopia simu wakati wa matangazo yaliyorushwa mbashara yalichukuliwa kuwa ni "matusi" na "kashfa" na Mamlaka Kuu ya Mawasiliano (HAC), ambayo ilisimamisha Redio Kayira Kolondieba kwa miezi mitatu.

Hatimaye, Boubacar Traoré, mhariri wa gazeti la L'Empire, anazuiliwa tangu Novemba 14. Anashtakiwa na mahakama ya kupambana na uhalifu wa mtandaoni kwa makala inayohusisha kampuni ya mafuta, Petro-Bama, katika muktadha wa marufuku ya mafuta ya wanajihadi. Kampuni hiyo imewasilisha malalamiko. Tarehe ya kesi bado haijulikani. Mwandishi wa habari atabaki gerezani hadi kesi yake itakaposikilizwa.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii