Zaidi ya wanafunzi 200 na walimu wa shule ya Kikatoliki wametekwa nyara

Idadi ya wanafunzi waliotekwa nyara katika shule ya Kikatoliki katika Jimbo la Niger, katikati mwa Nigeria, siku ya Ijumaa, Novemba 21, ilifichuliwa jioni y siku hiyo na Chama cha Wakristo nchini Nigeria (CAN): Wanafunzi 227 na walimu kutoka Shule ya St. Mary walitekwa nyara. Huu ni utekaji nyara wa pili wa aina hiyo nchini ndani ya wiki moja, baada ya wasichana 25 wa shule katika Jimbo la Kebbi, kaskazini magharibi kutekwa nyara.


"Kulingana na taarifa zetu, wanafunzi 215 na walimu 12 walitekwa nyara na magaidi" katika shule hii katika Jimbo la Niger, CAN imesema katika taarifa kufuatia ziara ya kiongozi wa chama kwa Jimbo la Niger, Bulus Dauwa Yohanna katika shule hiyo. "Wakati wa shambulio la kigaidi, baadhi ya wanafunzi walifanikiwa kutoroka," ameongeza katika taarifa hiyo.

Mapema siku hiyo, vyombo vya habari vya ndani viliripoti kutekwa nyara kwa wanafunzi 52 walio kati ya umri wa miaka 12 na 17. Serikali ya Jimbo la Niger ilithibitisha shambulio hilo katika Shule ya St. Mary lakini haikutoa idadi maalum.

Kulingana na mamlaka za eneo hilo, shule hiyo ilikuwa imepuuza agizo rasmi la kufunga shule kutokana na ripoti za kijasusi za utekaji nyara katika shule hiyo.

"Serikali ya Jimbo la Niger imepokea taarifa mbaya za kuhuzunisha kuhusu kutekwa nyara kwa wanafunzi wa Shule ya St. Mary katika manispaa ya Agwara," Gavana Mohammed Umaru Bago alitangaza mnamo Novemba 21, 2025, katika taarifa kwenye mitandao ya kijamii. "Idadi kamili ya wanafunzi waliotekwa nyara bado haijathibitishwa, huku vyombo vya usalama vikiendelea kutathmini hali hiyo," aliongeza kuhusu utekaji nyara uliotokea magharibi mwa Nigeria.

Mfululizo wa visa vya utekaji nyara

Chini ya wiki moja baada ya utekaji nyara wa Maga katika Jimbo la Kebbi, utekaji nyara huu wa pili wa watu wengi katika Shule ya St. Mary huko Papiri unaonyesha wazi udhaifu wa usalama na kimfumo ambao Nigeria inakabiliwa nao, anaripoti mwandishi wetu huko Abuja, Moïse Gomis. Watekaji nyara waliosawazishwa kikamilifu walifika katika kijiji. Walikwenda kutekeleza kitendo hicho kiovu bila vikwazo vikubwa katika msafara wa gari la kubeba mizigo na pikipiki zipatazo sitini, injini zikinguruma, kuelekea shule ya bweni iliyolengwa.

Na katika kipindi cha chini ya saa moja, wanaume wenye silaha waliwateka wasichana wengi na walimu wao kabla ya kukimbilia msituni. Rais Bola Ahmed Tinubu alibaki Nigeria, akifuta safari yake kuelekea nchini Afrika Kusini kuhudhuria mkutano wa kilele wa G20. Anafuatilia matukio yanayoendelea ya mgogoro huu mkubwa katika Jimbo la Niger, bila shaka, lakini pia huko Kebbi, ambapo wanafunzi 25 Waislamu walitekwa nyara wakiwa shuleni. Bila kusahau Kwara, ambapo waumini 35 walitekwa nyara wakati wa Misa. Hata hivyo, Atiku Abubakar, mpinzani wake mkuu, anabainisha uwepo wa rais hautoshi. Makamu wa rais wa zamani anahimiza serikali ya shirikisho kutangaza mara moja hali ya hatari kutokana na ukosefu wa usalama uliopo nchini.

Shule nyingi kote nchini zilifungwa. Utekaji nyara katika Jimbo la Niger ulifanywa kwa njia ya kushangaza, na hofu imetanda na kuenea katika majimbo mengine. Jimbo la Katsina, kaskazini mwa Nigeria, na Jimbo la Plateau, katikati, yalitangaza siku ya Ijumaa kufungwa kwa shule zao zote za msingi na sekondari.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii