Katika jamii ya leo,matukio ya vijana kuwanyanyasa wake zao yanaonekana kuongezeka na kusababisha uharibikaji wa ndoa nyingi.
Huku chanzo cha tatizo hili sikitu kimoja bali ni mchanganyiko wa sababu kadhaa.
Kwanza ,malezi duni huwafanya baadhi ya vijana kukua bila kujifunza heshima ,uvumilivu,nanamna ya kudhibiti hasira.
Pili,kukukosa maadili ya kibinadamu kama uaminifu ,uwajibikaji ,na mawasiliano bora huchangia wanaume kutumia nguvu kutatua migogoro,vilevile kukosekana kwa misingi imara wa maadili ya dini humaanisha vijana hawafuati mafundisho ya upendo ,utu,na amani ambayo dini nyingi zinahimiza.
Sababu nyingine ni shinikizo la kiuchumi,ambalo huongeza msongo wa mawazo na kupelekea baadhi ya wanaume kuonyesha hasira kwa familia zao.
Pia ,ukosefu wa elimu ya ndoa husababisha vijana kuingia kwenye mahusiano ya kudumu bila uelewa wa majukumu ,mawasiliano,na namna ya kutatua changamoto.
Ili kupunguza tatizo hili, ni muhimu kuimarisha malezi yenye maadili ,kutoa elimu ya ndoa ,kukuza heshima na uadilifu,pamoja na kuwasaidia vijana kiuchumi.
Makanisa ,misikiti ,shule na jamii kwa ujumla zinapaswa kushirikiana kuhamasisha ndoa zenye upendo na usawa.
Kupitia malezi bora,elimu na maadili imara,tunaweza kujenga familia salaama na kuimarisha jamii nzima.
NB: Mwandishi mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wakagera,nimzoefu katika semina za vijana sehemu mbalimbali Tazania.Tumia andiko hili kuwasaidia vijana walio kwenye ndoa na wanaotarajia.
#Familiamoja #AhsantekwaTime