Prof, Kabudi aagiza waandishi na wachapaji wa vitabu kuunda Shirikisho

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi ametoa agizo kwa Waandishi na Wachapishaji wa Vitabu kuunda Shirikisho ili waweze kuongeza sifa za kupata mikopo kwa urahisi kwa ajili ya kukuza mtaji wa kazi hizo.

Aidha Prof. Kabudi alisema hayo Novemba 21, mwaka huu jijini Dar es Salaam, wakati akifungua Maonesho ya 32 ya Vitabu yaliyoandaliwa na Umoja wa Wachapishaji Tanzania (PATA), akiwapongeza kwa jitihada walizonazo za kuhamashisha jamii kusoma vitabu ili kuongeza maarifa.

"Usomaji wa vitabu unaongeza maarifa, uwezo wa kufikiri, ufasaha wa lugha, kupunguza msongo wa mawazo na kuongeza Maadili" alisisitiza Prof. Kabudi.

Vilevile, aliwataka wadau hao wa vitabu kuweka mkazo katika ubora wa maudhui, kuheshimu hakimiliki za waandishi, kuimarisha kazi za tafsiri na kuhakikisha vitabu vinavyotolewa vinawiana na viwango vya kimataifa. 

#Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii