Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameanza ziara ya kiserikali nchini Gabon siku ya Jumapili, Novemba 23, yenye lengo la "kuimarisha na kufufua" ushirikiano wa pande mbili, miaka miwili baada ya kumalizika kwa utawala wa familia ya Bongo.
Hii ni ziara ya kwanza ya rais wa Ufaransa tangu Brice Oligui Nguema aingie madarakani. Rais wa Ufaransa alitua Libreville alasiri kwa ajili ya awamu ya tatu ya ziara hii barani Afrika, iliyoanzia Mauritius na Afrika Kusini, kabla ya kuelekea Angola siku ya Jumatatu. Alilakiwa kwenye uwanja wa ndege wa Libreville na Rais wa Gabon Brice Oligui Nguema, aliyechaguliwa mwezi Aprili baada ya mpito wa kisiasa wa miezi 19.
Huko Libreville, mji mkuu wa Gabon, wakuu hao wawili wa nchi walifanya mazungumzo katika Ikulu ya rais na kutoa taarifa ya pamoja kwa vyombo vya habari. Kuanzia mwanzo wa hotuba yake, Brice Clotaire Oligui Nguema alitoa shukrani zake za dhati kwa "msaada wa pande nyingi ambao Emmanuel Macron alitoa kwa nchi yake wakati wa mpito wa kisiasa. Lakini usaidizi huu si wa upande mmoja. Ufaransa na Gabon zinahitajiana," alibainisha.
Gabon imeanza mabadiliko makubwa ya kiuchumi, yaliyolenga kukuza rasilimali zake. Hatutaki tena kufanya mambo jinsi tulivyofanya hapo awali.
Mkuu wa nchi wa Gabon alimkaribisha kwa furaha kubwa sana mwenzake wa Ufaransa. Mnamo Novemba 23 huko Libreville, Emmanuel Macron alikaribishwa kwa mizinga 21, gwaride la kijeshi la dakika 30. Hizi zilikuwa heshima kubwa kwa ziara hii fupi.
Katika hotuba yake, rais wa Ufaransa alijibu hisia za mwenyeji wake. "Ufaransa imeunga mkono mpito tangu mwanzo," alisema mkuu wa nchi wa Ufaransa, ambaye alibaini kwamba Agosti 30, 2023, tarehe ambayo Oligui Nguema alichukua madaraka, "ilifungua enzi mpya nchini Gabon." Rais wa Ufaransa leo almekaribisha hitimisho na kukamilika kwa mpito wa kisiasa. Viongozi hao wawili kisha walijadili kwa kina masuala ya kiuchumi ya uhusiano wao. Wakati huo huo, ujumbe wa biashara ulifika Gabon ukiambatana na Emmanuel Macron.
Leo asubuhi, Rais Brice Oligui Nguema anatarajiwa kuendesha gari litakalomchukua Emmanuel Macron katika ziara yake katika wilaya ya Baie des Rois, mradi mkubwa wa kuendeleza ukingo wa maji wa Libreville.
Ziara ya rais wa Ufaransa imevutia umakini mkubwa wa vyombo vya habari. Hata hivyo, raia wengi wa Gabon haswa katika mitaa ya Libreville wanasema hawana imani na ushirikiano huu wa pande mbili, ingawa baadhi bado wana matumaini.
Ni lazima isemwe kwamba, machoni pa umma, watu wengi hawakuridhika kwa kiasi fulani kwa sababu wamehoji ushirikiano huu "utawaletea nini". "Lakini tunatarajia utawanufaisha nchi zote mbili."
Anges Kevin Nzigou wa chama cha FDS, ambaye sasa ni mfuasi wa Rais Brice Oligui Nguema, anaamini kwamba ziara hii kwa kweli ni mwendelezo wa uhusiano wa muda mrefu kati ya Ufaransa na Gabon. Kwake, ziara hii si jambo la kawaida. Anasema uhusiano huo ni wa pande zote mbili. Sio Emmanuel Macron pekee anayekuja kukamilisha mpito, lakini pia Brice Oligui Nguema ambaye anamkaribisha kwa furaha kubwa katika ukanda huo.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime