Mwanaume mmoja auawa na kundi la watu katika kituo cha ununuzi cha Mururi eneo Bunge la Gichugu akaunti ya kirinyanga baada ya kukamatwa akiiba kuku walioandaliwa kwaajili ya kusherehekea Krismas.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na wakazi wa Kijiji hicho wamedai kuwa kisa hicho kilitokea majira ya saa mbili asubuhi wakati mtuhumiwa alipoonekana ndani ya boma la msimamizi wa Kijiji.
Aidha wakazi wanadai kuwa baada ya mwanaume huyo kukamatwa wananchi wenye hasira kali waliripotiwa kununua mafuta kwenye kituo karibu na saa 24 na kumchoma moto mtuhumiwa huyo kabla polisi hawajafika eneo la tukio
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime