Tshisekedi, Kagame wasaini mkataba wa kumaliza vita

Rais Donald Trump wa Marekani amewapongeza viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Felix Tshisekedi na Rais wa Rwanda Paul Kagame kwa ujasiri wao wa kusaini mkataba wa amani unaolenga kumaliza mzozo wa Mashariki mwa Kongo.

Akizungumza kabla ya kutiwa saini kwa makubaliano hayo Trump alisema kuwa imekuwa siku  nzuri kwa bara la Afrika na dunia nzima kuonyesha  utawala katika  kufanikisha jambo ambalo wengi walishindwa kulitekeleza.

Aidha mkataba huo umetiwa saini mjini Washington na unalenga kuhitimisha miongo kadhaa ya machafuko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Kwa mujibu wa Trump hatua hiyo itafungua fursa za upatikanaji wa hifadhi ya madini muhimu ya Kongo kwa Marekani na kampuni zake.

Ingawa taarifa zinaonyesha kuwa mapigano bado yanaendelea mashariki mwa Kongo kati ya jeshi na makundi ya waasi, Trump alisisitiza kuwa matokeo ya mkataba huo yatashuhudiwa “haraka sana.”

Pamoja na kusifiwa na Ikulu ya White House kama makubaliano ya kihistoria mkataba huo unakuja baada ya miezi kadhaa ya jitihada za kidiplomasia zilizohusisha Marekani Umoja wa Afrika na Qatar.

Hata hivyo katika hafla ya kutia saini iliyodumu takribani dakika 50 Kagame na Tshisekedi hawakutazamana wala kupeana mkono, ishara ya mvutano uliopo kati ya nchi hizo mbili.

Rais Kagame alimpongeza Trump kwa hatua yake ya kujaribu kurejesha utulivu, huku Rais Tshisekedi akieleza matumaini yake kuwa mkataba huo hautakuwa ndoto, bali mwanzo wa amani ya kudumu.

Pamoja na matumaini hayo wachambuzi wanasema mkataba huo unaendelea kukabiliwa na hatari ya kufeli, kutokana na historia ndefu ya mapigano mashariki mwa Kongo, ambako zaidi ya makundi 100 ya kivita yanaendesha shughuli zake. Miongoni mwao, kundi lenye nguvu zaidi ni waasi wa M23.

Kwa miaka mingi, mashariki mwa Kongo imekuwa kitovu cha mapigano, lakini pia eneo lenye utajiri mkubwa wa madini adimu,

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii